Learning by Ear Once upon a time... in Africa Episode One: CRADLE OF MANKIND Author: Marta Barroso Editors: Maja Braun, Jan-Philipp Scholz CHARACTERS : Intro/Outro (female/male) Scene 1: Mum (38, female) June (13, female) Grandpa (77, male) Scene 2: June (13, female) Linda (13, female) Scene 3: Grandpa (77, male) Mum (38, female) June (13, female) Dad (40, male) Scene 4: Mum (38, female) June (13, female) 1
Baby (1, male) Linda (13, female) Women (all ages) Men (all ages) Dad (40, male) Scene 5: June (13, female) Mum (38, female) Dad (40, male) Grandpa (77, male) Intro: Hujambo na karibu kwenye makala ya Noa Bongo Jenga Maisha Yako kwa jina Hapo Zamani Za Kale... Huko Afrika katika hadithi hii mpya, kuhusu historia ya Afrika, tutaandamana pamoja na June na familia yake. June ni msichana mwerevu shuleni lakini pia anapenda sana kusikiliza hadithi za babu yake mzee Peter badala ya kumsaidia mama yake. Babu Peter ni mwandishi wa habari aliyestaafu, anazifahamu hadithi za nyakati mbalimbali. Emily, mama yake June, anafanya kazi zote za nyumbani, anawaangalia kuku na mbuzi pia. Francis na Stephen ni kaka zake June wakubwa, wanafanya kazi katika mji wa Bonairi kwa ajili ya kupata fedha za kuisaidia familia. Baba yake anaitwa, Charles,ni mkulima anafanya kazi shambani kutoka jua linapokucha hadi linapokuchwa. Tunayaangalia maisha ya sasa ya familia hiyo, katika kijiji cha Mbazi, hadithi za babu zinaelezea nyakati tafauti katika historia ya Afrika. Katika sehemu hii ya kwanza, June anasherehekea mwaka wake wa 13, 2
anataka kusikia kutoka kwa babu yake iwapo hapo zamani watoto walisherehekea siku zao za kuzaliwa. Jiunge nasi ili upate kujua maisha ya mwanadamu yalikoanzia, hapo zamani za kale Music 1, then cross fade with SFX First Scene: In the kitchen late afternoon. SFX: Kitchen (pots, fire); in the background: chickens, goats, birds, then fade under 1. Grandpa: Singing Happy Birthday song (June giggling) 2. Mum: (from a distance) Njoo, hebu njoo! Tutaimba baadae! June, hebu njoo uwashe moto, na mimi ninashughulikia kuku! Hata ingawa ni siku yako ya kuzaliwa, lakini haimaanishi kuwa huwezi kusaidia kazi za nyumbani! Alaa! Cross fade of mum s voice with June talking to Grandpa 3
3. June: Babu, hivi babu yako alikuwa pia anakupigia hadithi wakati ulipokuwa na miaka 13? 4. Grandpa: (laughing) Ndio, mjukuu wangu! Na hivyo ndivyo habari zilivyoweza kuenea wakati huo! 5. June: Na mambo yalikuwaje wewe ulipokuwa na miaka 13? 6. Grandpa: Oh, mambo yalikuwa tofauti kabisa wakati huo! 7. June: Kweli? Na je wakati babu yako alipokuwa na miaka 13, mambo yalikuwa tofauti pia? Na je wakati wa babu yake na wakati wa babu mzaa babu yake,na pia wakati wa babu mzaa babu (shocked) aliyemzaa babu ya babu yake, ilikuwaje wote hao walipokuwa na miaka 13? Na kabla ya hao? Na zamani, sana kabla ya hao? (laughs) 8. Grandpa: Kalba yao, na kabla ya hapo, yaani zamani, sana mambo yalikuwa tofauti sana wakati wa! Lucy Unamjua huyo Lucy alikuwa ni nani? (June: Hmhm!, like saying No ) Lucy ni mabaki ya kiumbe wa zamani yaliyovumbuliwa, ni kiumbe ambacho kilimtangulia mwanadamu. Inasemekana kuwa kiliishi takriban miaka milioni tatu 4
iliyopita. Na kwa sababu Lucy aliishi nchini Ethiopia, ndio maana bara la Afrika linaaminika kuwa ndio chanzo cha utu, mahala ambapo ubinadamu ulikoanzia! 9. June: Iooohhhh! Kweli?! (pause) babu, Je utachinja kuku, ili mama apike halafu sote tule kwenye birthday yangu,je. ingekuwaje kama tungeishi kwenye enzi za zamani, sana kama ule wakati wa Lucy? 10. Grandpa: Kama tungeliishi wakati wa Lucy, hata tusingesherehekea siku yako ya kuzaliwa, mjukuu wangu! 11. June: (disillusioned) Haiwezekani?! 12. Grandpa: Hebu fikiria leo sio leo ila zamani, za kale. Tuseme tuko kwenye enzi ya mawe, ambayo ilikuwa miaka kama milioni moja baada ya huyo Lucy kuishi Ethiopia! (pause) kama ungeliishi kwenye enzi hiyo ya mawe, usingekuwa na mtu ambaye angelikutolea hadithi. Na unajua ni kwa nini? 13. June: (curious) Ni kwa nini, Babu? 14. Grandpa: (whispering) Kwa sababu, ijapokuwa wewe bado ni mdogo, wakati ule ungelikuwa kama 5
mtu mzima, ungelifanya kila kitu ambacho watu wazima wangelikifanya kambini kwenu. 15. June: (whispering) Babu, hebu niambie: Je. June wa enzi ya mawe, nae alikuwa na mama ambaye kila mara alimwambia fanya hivi au fanya vile? 16. Grandpa: (serious) Mjukuu wangu, heshima kwa wakubwa ni kitu cha muhimu sana! 17. June: (serious) Samahani Babu 18. Grandpa: Mtazame, June wa enzi ya mawe na sasa anatembea na rafiki yake rafiki yako mpendwa anaitwa nani vile? 19. June: Linda! 20. Grandpa: Sawa, anakwenda na rafiki yake wa enzi ya mawe Linda kuchota maji kutoka mtoni kwa sababu wanataka kupika chakula. Njiani, wanaokota matunda, kwa kawaida Flashback Music Second Scene: On the way to the river. 6
SFX: Footsteps of two people on gravel path, meditative murmurs, footsteps stop, someone stirring in the bush. In the background: birds, then fade under 21. June: Hummm ajabu! Wakati kama huu huwa kuna matunda yaliyoiva 22. Linda: Ni kweli, June! (worried) kwa hivyo tutachukua nini kwa ajili ya kula? Kama baba na kaka zetu hawatarudi kutoka kuwinda, tutaishiwa na chakula! SFX: Someone slowly stirring in the bush, picking some fruit. In the background: birds, then fade under 23. June: Linda, usijifadhaishe moyo! Tuokote matunda haya halafu tutafute mizizi. Tunaweza pia kukamata wadudu! Hatutakufa kwa njaa, wee, utaona! SFX: Someone slowly stirring in the bush, picking some fruit. In the background: birds, then fade under 7
24. Linda: (surprised) Hebu angalia tunda hili! Sijawahi kuiiona hata mara moja! Tunaweza kulionja 25. June: Hapana, Linda! Ni vyema tuyachukue halafu tukamuonyeshe Etu tukifika kambini. Yeye anafahamu zaidi tunachoruhusiwa kula. 26. Linda: Hapo umesema kweli! Haujapita muda mrefu tangu mtu mmoja alipokufa kwa kula kitu kilichokuwa sumu SFX: Someone slowly stirring in the bush, picking some fruit. In the background: birds, then fade under 27. Linda: Kwa hivyo,kila kitu tunacho! Twende sasa mtoni! 28. June: (laughing) Haya twende, tushindane! Atakae fika mwanzo, atapata tunda! SFX: June running, Linda approaches, then two people running, then stop. In the background: birds, then fade under 29. June: (laughing, breathless) Inaonekana kama 8
vile, mto unazidi kusogea mbali kila siku! 30. Linda: (breathless) Ndio! Kabla ya wanaume kutoka kwenda kuwinda, nilimsikia mama yangu akisema kuwa mto umeanza kukauka... Flashback Music Third Scene: At home late afternoon. SFX: Kitchen (pots, fire). In the background: chickens, goats, birds, then fade under 31. Grandpa: Baadae, June na Linda wanaoga mtoni na kurudi kambini. Vile vile wanaume, waliokuwa wameenda kuwinda kwa muda mrefu nao wanarudi... 32. Mum: (from a distance) Baba, huoni kwamba hadithi zimetosha kwa leo? 33. June: (speaking loudly) Maa-mmma!!! Bado kidogo! (talking to grandpa) Babu, kwa nini iliitwa enzi ya mawe? 9
34. Grandpa: Kwa sababu wakati huo wanadamu walianza kutengeneza vifaa vyao kwa kutumia mawe. Walitumia mbao, mifupa, kola lakini jiwe ndio lilikuwa malighafi ya kisasa katika enzi hizo! Enzi ya mawe ni mojawapo katika nyakati zilizotangulia kwenye historia. 35. June: (proud) Ni mwanzo uliotangulia kabla ya historia, si ndio babu? (Grandpa: Hmhm!, like saying Yes ) kwa sababu wanadamu hawakujua kuandika wakati huo! 36. Grandpa: Haswa! 37. June: Ulikuwa ni wakati gani huo babu? Lazima itakuwa ni zamaaaani sana! 38. Grandpa: Naam! Inasemekana ilianzia Afrika kama miaka milioni mbili na nusu iliyopita. 39. June: Babu, kama Lucy aliishi Ethiopia, Je. June wa enzi ya mawe naye aliishi wapi? 40. Grandpa: Inawezekana, hata wewe pia uliishi huko huko Ethiopia, SFX: Door opens, footsteps, door closes, footsteps coming closer, 10
kitchen (pots, fire). In the background: chickens, goats, birds, then fade under 41. Mum: Charles! Nafurahi umerudi nyumbani! Hebu mwambie mtoto wako aje akaange ndizi! 42. Dad: Ah, mke wangu, leo ni siku yake ya kuzaliwa! Siku moja katika mwaka! (amused) na unajua chakula kinavyotokea June akipika! (talking to Grandpa) Hujambo, Baba! 43. Grandpa: (from a distance) Habari za jioni, Charles! SFX: Footsteps coming nearer, then stop, kitchen (pots, fire). In the background: chickens, goats, birds, then fade under 44. Dad: Habari nzuri, mzee Peter! (talking to June) mwanangu mpenzi, happy birthday! (kisses June) naona kuwa unasikiliza hadithi za babu mmeninyima nini? 45. June: Baba! Kaa hapa. Sasa umejiunga nasi kwenye hadithi! (happy) endelea, babu! SFX: Dad sits down, tired, murmuring, kitchen (pots, fire). In the 11
background: chickens, goats, birds, then fade under 46. Grandpa: Ni kama nilivyosema (amused) tuko kwenye enzi ya mawe! Na wanaume ndio wanawasili katika kambi... Flashback music Fourth Scene: At the camp. SFX: A baby cries out. In the background: women talking, birds, then fade under 47. Mum: June, je, kinywaji tayari umeshamaliza kutengeneza? Nduguyo mdogo anatakiwa ale kitu! SFX: Someone scraping two stones on one another. In the background: women talking, footsteps, birds, then fade under 48. June: Hapana, Mama! Bado ninajaribu kuwasha moto! Nitakuletea kinywaji haraka 12
nitakapoweza! 49. Linda: (shouting, from a distance, enthusiastic) Ndio hao! Wanaume wamesharudi! June stands up and runs to join Linda SFX: Footsteps running on gravel path. In the background: women talking, footsteps slowly approaching on gravel path, birds, then fade under 50. June: (shouting from a distance) Hiihhh, mama! Wamebeba mnyama ambae sio wa kawaida! SFX: Footsteps from various people slowly approaching on gravel path, pulling an animal. In the background: women talking, birds, then fade under Men murmuring, tired June runs to join the men SFX: Footsteps running on gravel path. In the background: footsteps slowly approaching on gravel path, women talking, birds, then fade under 13
51. June: Baba, ninafurahi uko hapa. Mtoto ana njaa! 52. Dad: (worried, meditative) sasa hivi sote tutakula, mwanangu! SFX: Footsteps from various people slowly approaching on gravel path, pulling an animal, then stop. In the background: women and men talking, birds, then fade under 53. Mum: Huhhh, mbona sura hiyo, mume wangu! Mambo hayakwenda viruzi mawindoni nini? 54. Dad: Yalikuwa magumu sana, mke wangu! Wanyama wameondoka. Hatukuwa na chochote cha kula kwa siku kadhaa! (Mum: Hmhm!, like saying Yes ) Mambo yakiendelea hivi, mtoto atashikwa na njaa tena! 55. Mum: Kwa hiyo, umeamua kufanya nini? 56. Dad: (sighing) Ah, mke wangu, mke wangu! (pause) itatubidi tuondoke tukatafute mahala ambapo pana maji yanayotiririka mtoni na palipo na wanyama wengi! Kesho 14
tutaondoka! Flashback music Fifth Scene: At home in the evening. SFX: Kitchen (pots, fire, kerosene lamp, bananas frying). In the background: crickets, then fade under 57. June: Babu, kwa nini wataondoka na wanaume wameleta mnyama kwa ajili ya chakula? 58. Mum: (from a distance) June! 59. Dad: (speaking loudly) mke wangu, achana na mtoto! Hebu mpe muda kidogo tu! 60. Mum: (from a distance, muttering) Ni kama nilivyosema. sina mtu wa kunisaidia 61. Grandpa: Lakini ni kwa muda gani mnyama huyo mmoja atatosheleza kambi nzima kwa chakula? Usisahau kuna watu karibu 30 wanaoishi hapo pamoja! 15
62. Mum: (from a distance) Umemaliza? (Pause) June! 63. Grandpa: (speaking loudly) Ndio, tumemaliza! (talking to June) sasa, nenda ukamsaidie mama, vinginevyo hatutapata chakula cha usiku! Outro: Na mpaka hapo ndio tumekamilisha sehemu ya kwanza ya hadithi kwa jina Hapo zamani za kale huko Afrika makala mpya katika Noa Bongo Jenga Maisha Yako kuhusu Historia ya Afrika! Je unafikiriaje wakati wa enzi ya mawe maisha yalikuwa rahisi kuliko sasa au vipi? Kumbuka unaweza kukisikiliza tena kipindi hiki au vipindi vingine vya Noa Bongo Jenga Maisha Yako, unaweza pia kutuandikia maoni yako. Tembelea mtandao wetu. Anuani yetu ni: w w w. d w w o r l d. d e / l b e Hadi wakati mwingine. Kwaheri! 16